UINGEREZA-WATALII-FEDHA-DUNIANI

Kampuni kubwa ya kitalii nchini Uingereza yafilisika

Ndege inayowasirisha watalii  kutoka kampuni ya  Thomas Cook
Ndege inayowasirisha watalii kutoka kampuni ya Thomas Cook REUTERS/Paul Hanna/File Photo

Kampuni kubwa ya Uingereza Thomas Cook ambayo imekuwa ikihusika na safari za watalii katika maeneo mbalimbai ya dunia na safari za angaa imefilisika.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imesababisha kukwama kwa watalii wengi waliokuwa wanagetemea huduma za kampuni hiyo, baada ya mazungumzo ya dakika za lala salama, kuoikoa  kutozaa matunda.

Mamlaka ya safari za angaa nchini Uingereza, imetangaza kuwa huduma za ndege za Shirika hilo zimesitishwa mara moja.

Ripoti zinasema kuwa watu zaidi ya 22,000 watapoteza kazi kote duniani kutokana na hili huku maelfu ya watalii hasa kutoka nchini Uingereza wakikwama katika maeneo waliyokuwa wamekwenda kutaliii.

Hata hivyo, Waziri wa uchukuzi nchini Uingereza Grant Shapps amesema kuwa utaratibu unafanyika ili kuwarudisha watalii waliokwama nyumbani bila malipo yoyote.

Kampuni hii ambayo imekuwa bora duniani katika huduma za utalii ilianzishwa mwaka 1841 lakini madeni mengi yameifanya ifilisike.