MEXICO-SIASA-PAPA FRANCIS-NGONO

Watoto 175 walifaniwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono nchini Mexico

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis REUTERS/Yara Nardi

Ripoti mpya kutoka ndani ya kanisa Katoliki imeonesha kuwa karibu watoto 175 walifaniwa vitendo vya udhalilishaji wa kingono na wachungaji kutoka tawi la kanisa hilo nchini Mexico.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imemtaja muasisi wa kanisa la Legionaries of Christ, Marcial Maciel, kuwadhalilisha watoto zaidi ya 60 huku mapadri na mashemasi 33 wakikiri kufanya vitendo hivyo kuanzia mwaka 1941.

Matokeo ya uchunguzi huu uliokuwa ukifanywa na tume maalumu iliyoundwa mwezi Juni mwaka huu, imetazama vitendo vilivyofanywa kuanzia mwaka 1941 hadi December 16 mwaka huu.

Ripoti imesema watoto waliofanyiwa vitendo hivi wengi walikuwa ni wavulana wa kati ya miaka 11 hadi 16, huku viongozi 18 kati ya 33 walioshiriki kufanya vitendo hivi wakisalia kuhudumu mpaka sasa.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu hata hivyo yameendelea kulikosoa kanisa katoliki kwa kushindwa kuchukua stahiki dhidi ya wahusika wake wanaoendelea kutoa huduma.