SAUDI ARABIA-JAMAL-SIASA-MAUAJI

Watu watano walioshtakiwa kumuua Jamal Khashoggi wahukumiwa kifo

Mahakama nchini Saudi Arabia imewahukumu kifo watu watano na kuwafunga jela wengine watatu, kwa kosa la kuhusika na kifo cha mwandishi wa Habari Jamal Khashoggi, mauaji ambayo yalishtumiwa kimataifa. 

Mwandishi wa Habari wa Saudi Arabia aliyepoteza maisha  Jamal Kashoggi
Mwandishi wa Habari wa Saudi Arabia aliyepoteza maisha Jamal Kashoggi REUTERS/Osman Orsal/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Khashoggi, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Saudi Arabia aliyeandikia Gazeti la Washington Post aliuawa ndani ya ubalozi mndogo wa Saudi Arabia jijini Instanbul nchini Uturuki, mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Pamoja na hilo, Mahakama imewaondolea mashtaka wasaidizi wawili wa MwanaMfalme Mohammed bin Salma, waliokuwa wanashtumiwa kwa mauaji hayo, kwa ukosefu wa ushahidi.

Mamlaka ya Saudi Arabia imekuwa ikishtumiwa kwa mauaji hayi lakini imejitetea na kukanusha shutuma hizo huku ikiwakamata watu 11 ambao haikuwataja.

Kabla ya tangazo la leo kutoka Mahakamani, mtalaam wa umoja wa mataifa baada ya utafiti wake, alieleza kuwa, mauaji hayo yalitekelezwa kwa makusudi.

Khassogi aliauwa akiwa na umri wa miaka 59 na mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni wakati alipokuwa ameenda katika Ubalozi wa nchi yake nchini Uturuki.

Shirika la Kimataifa linalotetea wanahabari duniani RSF limesema haki imekanyangwa na kinachotokea ni kufunika ukweli kuhusu mauaji hayo.