VIRUSI-CHINA-WHO-WUHAN

Virusi hatari vyakwamisha shughuli katika mji wa Wuhan nchini China

Maafisa wa afya nchini China
Maafisa wa afya nchini China REUTERS/Stringer/File Photo CHINA OUT

Shughuli za kawaida katika mji wa Wuhan nchini China, wenye idadi ya watu karibu Milioni 11, zimesimama kwa muda kufuatia wasiwasi wa kusambaa kwa virusi vilivyopewa jina Corona, vinavyoathiri mfumo wa kupumua.

Matangazo ya kibiashara

Watu wanaoshi katika mji huo, wameshauriwa, kutoondoka makwao wakati huu mamilioni ya watu wakiahirisha safari zao kwa hofu ya kuambukizwa virusi hivyo.

Ripoti zinasema kuwa, virusi hivyo vimesambaa katika maeneo mengi ya nchi hiyo, huku visa vichache vikiripotiwa katika mataifa kama Marekani.

Hadi sasa watu 17 wamepoteza maisha na wengine 500 wameambukizwa, na kuleta kumbukumbu ya maambuzi mengine ya virusi kama hivi ambavyo vilisabisha vifo vya watu 800 miaka ya 2000.

Shirika la agya duniani WHO, linasema kuwa linafuatilia kwa karibu mlipuko wa vurusi hivo, kabla ya kuamua ikiwa ni tishio la dunia na hatua za kuchukua.