MABADILIKO YA HALI YA HEWA

Tabianchi: Miaka mitano baada ya Mkataba wa Paris, matokeo yaanza kuonekana

Maandamano ya hivi punde jijini  Sydney nchini Australia, 10 Januari 2020, kushinikiza mageuzi katika harakati za kuhifadhi mazingira
Maandamano ya hivi punde jijini Sydney nchini Australia, 10 Januari 2020, kushinikiza mageuzi katika harakati za kuhifadhi mazingira Tammy Gill

Viongozi wa dunia wanakutana leo kwa njia ya video kutatdhimini hatua iliyopigwa baada ya miaka mitano ya mkataba wa kihistoria wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ulioikiwa mjini Parsi, nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao pia wanatarajiwa kutangaza malengo mapana zaidi ya kudhibiti ongezeko la joto duniani.

Mkutano huu wa 21 wa Umoja wa Mataifa kuhusu mkataba wa kihistoria wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi, COP21, ulifanyika katika wilaya ya Le Bourget karibu na mji wa Paris mwezi Desemba 2015.

Wajumbe kutoka nchi 195, nyingi zikiwa ni kutoka Umoja wa Ulaya walishiriki mazungumzo kwa siku 15 katika vikao vya faragha ili kuweza kufikia mkataba.

Rais wa COP, Laurent Fabius, na balozi wa Ufaransa anayehusika na masuala ya tabia nchi, Laurence Tubiana, walifanya juhudi kubwa kushawishi nchi ambazo hutoa gesi nyingi chafu - nchi zilizowtawi kiviwanda na nchi zinazozalisha mafuta - kuhusika katika vita hivi, hata kama makubaliano yaliyofikiwa katika Umoja wa Mataifa ni matokeo ya makubaliano.

Mkataba wa Paris, uliopitishwa na nchi 55 zinazowakilisha 55% ya uzalishaji wa gesi chafu, ulianza kutumika Novemba 4, 2016 - ikichukua nafasi ya Itifaki ya Kyoto, ambayo ilimalizika mnamo mwaka 2012.