COVID 19-UMASIKINI

COVID-19: Oxfam yataka mataifa tajiri kusaidia mataifa masikini kifedha

Oxfam
Oxfam REUTERS/Andres Martinez Casares

Shirika la Kimataifa la Oxfam linalopambana na umasikini katika ripoti yake, linasema janga la COVID-19 na hatua ya mataifa mbalimbali kuwazuia watu kutembea, zimekuwa na madhara kwa mamilioni ya watu duniani.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Shirika hilo, inaeleza kuwa, hali hiyo inaelekea kusababisha mamilioni ya watu kuwa masikini, iwapo hatua za dharura hazitochukuliwa.

Mamilioni ya watu wamepoteza ajira kote duniani, huku wengine zaidi ya Bilioni Mbili na Laki Saba, wakiwa hawajapokea msaada wowote wa kifedha kuwasaidia kukabiliana na Mmkali ya COVID-19.

Imebainika kuwa, miongoni mwa mataifa nane kati ya 10 kote duniani, hayakuwajali raia wake, huku wanaothirika zaidi wakiwa ni wanawake wanaofanya kazi ndogondogo ili kulisha familia zao.

Ili kuepuka mamilioni ya watu kuzama kwenye dimbwi la umasiki, Shirika la Oxfam lenye makao yake nchini Uingereza, linayataka mataifa tajiri kuyasaidia mataifa masikini kifedha ili kuwasaidia raia wake wanaopitia kipindi kigumu kutokana na janga hilo.