KRISMASI

Wakristo duniani washerehekea Sikukuu ya Krismasi

Sikukuu ya Krismasi 2020
Sikukuu ya Krismasi 2020 Church of England

Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani Jumatatu hii, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo wakati dunia ikiandamwa na janga hatari la COVID-I9.

Matangazo ya kibiashara

Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.

Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi, lakini mwaka huu hali sio ya kawaida kutokana na virusi vya Corona vinavyosababisha ugoj-njwa hatari wa COVID-19 ambapo nchi kadhaa duniani ziko chini ya vizuizi vya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Mjini Bethlehem nchini Israel, mji ambao Wakiristo wanaamini kuwa Yesu alizaliwa, mwaka huu hakukushuhudiwa shamrashamra kama miaka ya nyuma.

Tayari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, alishatowa tamko la kuwataka waumini wa kanisa hilo kufuata maagizo yote ya mamlaka za kidunia juu ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Ibada maalum ya Krismasi kwenye uwanja maarufu wa Mtakatifu Petro, Basilica, ilirejeshwa nyuma - badala ya saa tatu na nusu usiku ikawa saa moja na nusu magharibi.

nchini Italia, viongozi wa makanisa wakameifanya sherehe ya mkesha kuanza mapema badala ya usiku wa manane kufuatia hatua ya serikali kuweka marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa nne usiku.