DUNIA-WANAHABARI

Wanahabari 50 wauawa mwaka 2020 wakiwa kazini

Shirika la Kimataifa linalotetea wanahabari la Reporters Without Borders.
Shirika la Kimataifa linalotetea wanahabari la Reporters Without Borders. AFP/Bertrand Guay

Wanahabari 50 na wafanyikazi mbalimbali wa vyombo vya Habari  waliuawa mwaka 2020 kutokana na kazi zao kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa linalotetea wanahabari la Reporters Without Borders.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Shirika hilo inaeleza kuwa idadi kubwa ya wanahabari hao waliuawa katika nchi ambazo hazina utovu wa usalama wala zisizo kwenye vita.

Miongoni mwa wanahabari waliolengwa na hata kuuawa ni wale wanaofanya ripoti za kiuchunguzi kuhusu makossa ya jinai, ufisadi na masuala ya mazingira.

Nchi ambazo zimeshuhudia kulengwa kwa wanahabari kwa mwaka 2020 ni pamoja na Mexico, India na Pakistan.

Aidha, RSF inaeleza kuwa asilimia 84 ya wanahabari waliouawa mwaka huu, walilengwa makusudi kutokana na kazi zao kinyume na asilimia 63, mwaka 2019.

Mwaka uliopita, wanahabari 53 waliuawa na RSF inasema kupungua kwa idadi hiyo mwaka huu ni kutokana na wanahabari wengi kutoripoti katika maeneo ya matukio kutokana na janga la Covid 19 lakini 387 wamefungwa jela kutoka na kazi zao.