WHO

COVID-19: Kamati ya dharura ya WHO kukutana kuhusu aina mpya ya Corona

Mkurugenzi Mkuu WHO  Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi Mkuu WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus REUTERS/Denis Balibouse

Kamati ya dharura ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inatarajia kukutana leo Alhamisi kuhusu aina mpya za Corona, ambazo zinawatia wasiwasi viongozi duniani, ambapo vita dhidi ya kuibuka tena kwa janga hilo vinaendelea kwa vizuizi dhidi ya janga hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kamati ya wataalam ya WHO, ambayo kawaida hukutana kila baada ya miezi mitatu, iliitishwa mapema wiki mbili.

Mapendekezo ya shirika la Afya Duniani, WHO, na nchi wanachama yatatolewa baada ya mkutano huo.

Kulingana na shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya nchi zinazokabiliwa na aina mpya ya kirusi cha Corona kilichoanzia nchini Uingereza imefikia hamsini na nchi 20 zinakabiliwa na kirusi cha aina hiyo kilichoanzia nchini Afrika Kusini.

Aina ya tatu ya kirusi cha Corona ambacho Japani ilitangaza Jumapili Januari 10 inaweza kuathiri jibu la kinga na kuna haja ya kuitathimini zaidi, kulingana na WHO, ambayo inabaini katika jarida lake la kila wiki "aina mpya ya Corona inayotia wasiwasi".

"Kadiri virusi vya SARS-CoV-2 vinavyoenea, athari inaendelea kuwa kubwa zaidi katika nchi mbalimbali duniani," imesema WHO.

"Viwango vya juu vya maambukizi vinamaanisha kwamba watu wanapaswa kutarajia hali mbaya zaidi kuibuka."