Siku ya wanawake Duniani : Mafanikio na changamoto wanazopitia wanawake Beni
Imechapishwa:
Machi 8 ni siku ya kimataifa ya wanawake. Idhaa ya Kiswahili ya RFI inaadhimisha siku hiyo kwa kuangazia masuala yanayowahusu wanawake katika maeno mbalimbali duniani, hususan katika wilaya ya Beni, mkoani Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.
Katika·siku·hii·ya·leo·ulimwengu·ukiadhimisha·siku·ya·wanamke·duniani·Idhaa·ya·Kiswahili·ya·RFI·inaangazia·mafanikio·na·changamoto·wanazopitia·huko·Mashariki·mwa·Jamhuri·ya·Kidemokrasia·ya·Congo,·wanawake·wengi·wamepoteza·waume·na·watoto·wao·kutokana·na·mashambulizi·yanayotekelezwa·na·makundi·ya·waasi.¶
Huko·wilayani·Beni,·wanawake·wengi·sasa·ni·wakimbizi·baada·ya·kuponea·mashambulizi·ya·waasi,wengi·wameeleza·changamoto·zao.¶
"Tulifika·hapa·baada·ya·kukimbia·mapigano·kati·ya·vikosi·vya·serikali·na·waasi,·mama·yangu·mzazi·sijuwe·wapi·alipo·mpaka·sasa,·na·hapa·ninaishi·na·watoto·wawili·mayatima·na·nina·zatoto·zangu·hapa·15·ambao.·Ninaishi·mazingira·magumu·kwa·kweli",·amesema·Kahindo·Élysée.¶
Siku·ya·Wanawake·Duniani·huadhimishwa·tarehe·8·Machi·ya·kila·mwaka.·Siku·hiyo·ilianza·kuadhimishwa·tarehe·8·Machi·1975·baada·ya·Umoja·wa·Mataifa·kuridhia·siku·hii·kutumika·kama·siku·rasmi·ya·kuikumbusha·dunia·juu·ya·haki·za·wanawake.¶
Siku·ya·wanawake·duniani·kwa·mara·wa·kwanza·ilisherehekewa·katika·mwaka·wa·1911·ambapo·mataifa·kumi·na·moja·yalikusanya·wanawake·mia·moja·walipoanza·kuadhimisha·siku·hii.·¶
Mwaka·1908·jumla·ya·wanawake·elfu·kumi·na·tano·waliandamana·katika·katika·mji·wa␣New·York·wakidai·kupunguziwa·muda·wa·kufanya·kazi·,kupata·ujira·wa·kuridhisha·na·kupewa·haki·ya·kupiga·kura.·¶
Mwaka·1909·mwanamke·kwa·jina·la·Clara·Zetkin·alipendekeza·kuanzishwa·kwa·siku·ya·wanawake·duniani·katika·mkutano·wa·wafanyakazi·wanawake·uliofanyika·katika·jiji·laCopenhagen·nchini·Denmark.·¶