Marekani, EU na Afrika Kusini zasitisha chanjo ya Johnson & Johnson

Hatua hiyo imesababisha Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson kusitisha usambazaji wa chanjo hiyo katika mataifa kadhaa ya bara Ulaya.
Hatua hiyo imesababisha Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson kusitisha usambazaji wa chanjo hiyo katika mataifa kadhaa ya bara Ulaya. AP - Mary Altaffer

Marekani, Umoja wa Ulaya na Afrika Kusini zimesitisha kwa muda utoaji wa chanjo aina ya Johnson & Johnson baada ya ripoti kuwa, baadhi ya watu waliopewa chonjo hiyo kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, kukumbwa na kuganda kwa damu mwilini.

Matangazo ya kibiashara

Nchini Marekani, hatua hii imekuja baada ya kikao cha watalaam wa afya na kupendeza kusitishwa kwa matumizi ya chanjo hiyo baada ya wanawake sita wenye umri kati ya miaka 18 na 48 waliokuwa wamechomwa sindano ya chanjo hiyo, kuganda damu mwilini siku 13 baada ya kuchomwa chanjo hiyo.

Mtu mmoja ambaye aliganda damu baada ya kuchomwa chanjo hiyo anaeleezwa kupoteza maisha.

Hatua hiyo imesababisha Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson kusitisha usambazaji wa chanjo hiyo katika mataifa kadhaa ya bara Ulaya.

Hatua hii inajiri baada ya mataifa kadhaa pia kusitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca kwa sababu kama hizo lakini shirika la afya duniani WHO linasema ni salama.