Corona yadhofisha uhuru wa vyombo vya habari duniani

Uhuru wa vyombo vya habari duniani umedorora kwa sababu ya janga la Corona
Uhuru wa vyombo vya habari duniani umedorora kwa sababu ya janga la Corona © PRAKASH SINGH/AFP

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani imeadhimishwa Jumatatu hi Mei 3, ikiwa ni haki ya kimsingi inayokabiliwa na vitisho zaidi duniani. Mtazamo huo unaungwa mkono na mashirika mbali mbali, kutoka Unesco hadi Shirikisho la Kimataifa la Wanahabari.

Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka (RSF), vitisho hivi  ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari ulimwenguni umepungua. Na moja ya vitisho vilivyoibuka mwaka jana ni janga la COVID-19.

"Ninafikiria mtu mmoja nchini Kenya ambaye anafanya kazi kwa Gazeti dogo," anasema Anthony Bellanger. Katibu mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Wanahabari (IFJ) hataki kumtaja jina lake kutokana na usalama wake. Mtu huyu alitaka kuchunguza hali ya afya katika nchi yake. Lakini alipata vitisho: barua pepe, ujumbe kwenye mitandao ya kijamii na kisha alikutana ana kwa ana na wanaomfanyia vitisho, mbele ya nyumba yake au nje ya ofisi.

Waandishi wa habari wanaofanya kazi kuhusu janga hilo wameonekana wakikamatwa kwa kuwekwa kizuizini kwa siku moja, mbili au tatu. "Hadi kukamatwa rasmi kwa kuhatarisha usalama wa taifa," anakumbuka Anthony Bellanger. Kwa ukosefu wa mashtaka na baada ya kuingiliwa kati na chama cha  Wanahabari wa Kenya, mwishowe aliachiliwa. Lakini alikamatwa tena siku chache baadaye, kwa sababu zile zile, kabla ya kuachiliwa tena.

Nchini Kenya wanahabari wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kukosa malipo yanayokidhi na pia unywanyasaji wa kingono dhidi ya wanahabari wa kike.