COVID-AFYA

Coronavirus: Dola bilioni 2.4 za ziada kwa mpango wa Covax zapatikana

Mpano wa Covax umetoa dozi milioni 77 kwa nchi 127 tangu mwezi wa Februari, lakini zimezuiliwa na masharti yaliyowekwa na India juu ya usafirishaji wa chanjo wakati mlipuko umeendelea kuathiri vibaya nchi hiyo.
Mpano wa Covax umetoa dozi milioni 77 kwa nchi 127 tangu mwezi wa Februari, lakini zimezuiliwa na masharti yaliyowekwa na India juu ya usafirishaji wa chanjo wakati mlipuko umeendelea kuathiri vibaya nchi hiyo. REUTERS - Tiksa Negeri

Siku ya Jumatano, nchi na wafadhili wa watu binafsi waliahidi karibu dola Bilioni 2.4 (sawa na euro Bilioni 1.96) kwa mpango wa kushiriki chanjo ya Covax, kupanua juhudi za kufanya chanjo dhidi ya COVID -19 kupatikana kwa watu wa nchi masikini zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Matangazo, kuanzia dola 2,500 kutoka Mauritius hadi mamilioni ya dola na dozi kutoka nchi tajiri, yalitolewa katika mkutano ulioandaliwa na Japan na mamlaka ya chanjo (GAVI), ambayo inaongoza mpango wa Covax pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Fedha hizi zitawezesha mpango wa Covax kupata dozi ya ruzuku bilioni 1.8 ambayo oitapelekwa kwa nchi zenye kipato cha chini mnamo mwaka 2021 na mapema mwaka 2022, ambayo itatosha kulinda 30% ya watu wazima katika nchi hizo, GAVI imesema katika taarifa.

Tumechukua hatua kubwa kuelekea "ulinsi wa dunia", amesema Jose Manuel Barroso, Mkuu wa GAVI. Fedha hizi mpya zinaleta jumla ya ufadhili wa mpango wa Covax hadi dola Bilioni 9.6, ameongeza.

Mpango wa Covax umetoa dozi milioni 77 kwa nchi 127 tangu mwezi wa Februari, lakini zimezuiliwa na masharti yaliyowekwa na India juu ya usafirishaji wa chanjo wakati mlipuko umeendelea kuathiri vibaya nchi hiyo.