UN-UTEUZI

Antonio Guterres kuwania muhula wa pili kama mkuu wa UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. AP - Maxim Shemetov

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura kumuunga mkono Antonio Guterres katika juhudi zake za kuwania awamu ya pili kama katibu mkuu wa umoja huo.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Usalama Jumanne limeidhinisha uungwaji wake mkono kwa muhula wa pili wa Antonio Guterres, 72, kuongoza umoja huo kati ya mwaka 2022 na 2026, kipindi ambacho atatarajiwa kuhusu utatuzi wa mizozo.

Antonio Guterre, Waziri Mkuu wa zamani wa Ureno, ambaye ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa tangu mwezi Januari 2017, alikuwa mgombea pekee kwenye nafasi hiyo. Karibu wagombea kumi wa kibinafsi hawakukubaliwa kwa sababu hawakuungwa mkono na moja ya nchi wanachama 193 wa umoja huo.

Katika kikao kifupi cha faragha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo ni muhimu katika mchakato wa uteuzi, lilikuwa na kauli moja kupendekeza kwamba Mkutano MKuu wa Umoja wa Mataifa umwongeze muda kiongozi wake, ametangaza rais wa sasa wa baraza hilo, Balozi wa Estonia Sven Jürgenson. Uthibitisho rasmi kutoka kwa Mkutano Mkuu wa Umja wa Mataifa unatarajiwa hivi karibuni.

Baada ya kipindi cha kwanza kujitolea kupunguza athari kubwa kwa kufanyika kwa sera ya upande mmoja ya Donald Trump, Antonio Guterres atalazimika kuwa na "mpango katika kupambana dhidi ya mizozo yote mikubwa", mwanadiplomasia mmoja amebaini.

Hadi kufikia sasa, rekodi yake imekuwa mbaya kwa miaka mitano, mizozo katika nchi za Syria, Yemen au Mali imebaki bila suluhisho la kisiasa. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Makedonia Kaskazini ameteuliwa na utulivu umeanza kupatikana nchini Libya, lakini Umoja wa Mataifa una jukumu kubwa zaidi la kuandamana na mchakato ulioanzishwa na Walibya.