Tovuti mbalimbali zilizoathiriwa kwa muda zaanza kufanya kazi

Makao makuu ya Gazeti la New York Times huko New York Machi 1, 2010.
Makao makuu ya Gazeti la New York Times huko New York Machi 1, 2010. REUTERS - Lucas Jackson

Tovuti mbalimbali za serikali, Habari na mitandao ya kijamii duniani, imeanza kufanya kazi tena baada ya saa kadhaa siku ya Jumanne, kutopatikana.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa tovuti hizo, zilizotoweka kwa muda ni pamoja na zile za Habari kama Le Monde la Ufaransa, New York Times la Marekani, Guardian, Financial Times zote za Uingereza, huku tovuti ya serikali ya Uingereza nayo pia ikiathiriwa.

Ripoti za awali zinaeleza kuwa tatizo hilo huenda lilitokana na kasoro katika mfumo wa kampuni ya Marekani Fastly, unaotoa huduma za kubeba mifumo ya tovuti kubwa duniani.

Hata hivyo, kampuni hiyo ya Fastly, imesema kuwa tatizo limegundulika na kufanyafiwa kazi, wakati huu tovuti hizo zinapoanza tena kufanya kazi.

Hitilafu hiyo imesababisha mjadala wa miundombinu mingi ya mtandao kumilikiwa na  kampuni chache, kwa hofu kuwa hali kama hii inapotokea, inasababisha usumbufu na hasara kubwa duniani.