Bilionea Branson, akamilisha safari ya kihistoria kwenda angani

Bilionea Richard Branson, akiwasalimia watu walijitokeza kuona akipanda chombo chake alichokitumia  kwenda angani. 11 Julai 2021.
Bilionea Richard Branson, akiwasalimia watu walijitokeza kuona akipanda chombo chake alichokitumia kwenda angani. 11 Julai 2021. © AP/Andres Leighton

Bilionea wa Uingereza, Richard Branson, hapo jana alisafiri kwa mara ya kwanza kwenda angani kwa kutumia chombo chake cha Virgin Galatic, safari aliyosema ya kihistoria katika maisha yake, tukio ambalo amesema huenda likafungua fursa za utalii wa angani.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza baada ya chombo hicho kurejea duniani, Branson, aliwapongeza wafanyakazi waliofanikisha utengenezaji wa chombo hicho na kuhakikisha safari yake pamoja na marubani wawili ilikuwa salama na mafanikio.

 

Chombo hicho kilisafiri umbali wa kilometa 85 kupita kiwango cha kawaida cha kwenda angani, kitendo kilichosaidia wasafiri waliokuwemo kushuhudia mandhari ya kipekee ya syari ya dunia.

 

Mafanikio ya safari yake, yanamfanya Branson, kuvunja rekodi ya bilionea mwenzake Jefff Bezos ya kuwa bilionea wa Kwanza kuvuka mstari wa chombo cha kibiashara kufika katika anga za juu.

 

Kupitia ukurasa Wake wa Twitter, Branson, amesema ni faraja kwake kuona anakuwa binadamu wa Kwanza kutimiza ndoto ya kwenda angani kwa kutumia chombo mfano wa roketi zinazotuliwa kwenda kwenye sayari.

 

Lakini msikilizaji wakati mabilionea hawa wakifanikisha haya yote, wadadisi wengi wanajiuliza ikiwa wanaona changamoto ambazo dunia inakabiliwa nazo ikiwemo za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwekeza fedha wanazotumia kuinusuru sayari ya dunia.