MICHEZO YA OLIMPIKI- JAPAN

Michezo ya Olimpiki yafunguliwa jijini Tokyo nchini Japan

Sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki jijini Tokyo nchini Japan, Julai 23 2021
Sherehe za ufunguzi wa michezo ya Olimpiki jijini Tokyo nchini Japan, Julai 23 2021 REUTERS - DYLAN MARTINEZ

Michezo ya Olimpiki iliyocheleweshwa kwa mwaka mmoja kutokana na janga la Covid  19, imeanza jijini Tokyo nchini Japan, michezo inayofanyika katika uangalizi mkubwa kutokana na janga hilo linaloendelea kuitesa dunia.

Matangazo ya kibiashara

Kinyume na miaka iliyopita, kwa sababu Michezo hii inafanyika, katikati ya janga la Covid 19, ni watu wachache tu ndio waliohudhuria sheria za ufunguzi.

Kiongozi mkuu wa Japan, Naruhito, rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Jill Biden, mke wa rais wa Marekani Joe Biden, ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioshuhudia ufunguzi wa michezo hiyo mikubwa duniani.

Michezo hii itafanyika katika uwanja mpya wa Taifa jijini Tokyo ambako wanamichezo zaidi ya 11,000 watashindana katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Maandalizi wa michezo hii, wamezuia watazamaji wa michezo hii kutoka nje ya nchi ya Japan kwa mara ya kwanza kutokana na janga la Corona.

Ni watazamaji wachache tu katika baadhi ya mashindano ndio watakaoruhusiwa kushiriki kwenye michezo hii mikubwa duniani.