WHO yaonya juu ya umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa

COVID-19 inaendele kusababisha vifo na maambukizi zaidi katika nchi mbalimbali.
COVID-19 inaendele kusababisha vifo na maambukizi zaidi katika nchi mbalimbali. AP Photo/Mark Schiefelbein

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekumbusha juu ya umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa kugundua chimbuko la janga la COVID-19, baada ya China kupinga uchunguzi wowote zaidi kwenye ardhi yake.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, Beijing ilikataa awamu ya pili ya uchunguzi wa WHO, ambayo inajumuisha kati ya hali zinazoweza kutokea kufuatia uzembe katika utendakazi katika maabara ya China.

Alipoulizwa juu ya mtazamo wa China wakati wa mkutano wa Umoja wa Mataifa huko Geneva, msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amesema: "Hii sio siasa, hakuna nafasi ya kulaumiana".

"Kwa kweli haya ni mahitaji ambayo tumewekewa: kujaribu kuelewa ni vipi vimelea vya magonjwa viliambukizwa kwa watu. Kwa maana hii, nchi zina jukumu la kufanya kazi pamoja na kufanya kazi na shirika la Afya Duniani katika hali ya ushirikiano" , ameoneza.