MAZINGIRA

Wanaharakati 227 wa mazingira wauawa duniani kote mwaka 2020

Wafuasi wa mwanaharakati wa mazingira Berta Caceres walikusanyika wakati wa kesi ya Roberto David Castillo huko Tegucigalpa, Honduras Jumatatu, Julai 5, 2021.
Wafuasi wa mwanaharakati wa mazingira Berta Caceres walikusanyika wakati wa kesi ya Roberto David Castillo huko Tegucigalpa, Honduras Jumatatu, Julai 5, 2021. AP - Elmer Martinez

Dunia kwa sasa iko katika hali mbaya na wakati mwingine wale wanaoitetea ndio wanalengwa katika visa mbalimbali. Mwaka jana, wanaharakati 227 wa mazingira waliuawa kote ulimwenguni. Haya ni kulingana na ripoti ya shirika la kimataifa la Global Witness.

Matangazo ya kibiashara

Mashambulio haya kila wakati yanahusishwa na visa vya unyonyaji mwingi wa maliasili na yamekithiri katika ukanda wa Amerika Kusini.

Colombia inashikilia rekodi ya kusikitisha ya mauaji ya watetezi wa mazingira, 65 waliuawa mwaka jana. Wengi walilaani unyonyaji mkubwa wa maliasili, katika maeneo ambayo makundi yenye silaha mara nyingi yanadhibiti. Watu wa asili wanalengwa hasa na mashambulizi hayo.

Louis Wilson, msemaji wa shirika lisilo la kimataifa la Global Witness, anaelezea kuwa "jamii za watu wa asili zinaathiriwa hasa katika nchi kama Colombia kwa sababu wao ni wasimamizi wa ardhi na,  wana ulinzi mdogo wa kisheria katika nchi kama Colombia. "

Katika Amerika Kusini, kama vile Asia au Afrika, wanaharakati wa mazingira wanauawa. Na katika idadi kubwa ya kesi, hakuna haki yoyote inayotendeka.

Itakumbukwa kwamba mwaka 2017 zaidi ya wanaharakati 200 wa mazingira waliuawa wakati mauaji hayo yaliyofadhiliwa na serikali yakihusishwa na miradi mikubwa iliyo na faida kutoka makampuni makubwa yakiongezeka.

"Wakati mahitaji ya bidhaa hizi dunaini yakiongezeka, kuna kinyang'anyiro miongoni mwa wafanyabiashara kujipatia kiasi kikubwa cha ardhi wanachohitaji ili kupanda mazao hayo", amesema Ben Leather, mtetezi mwandamizi kutoka Global Witness. Leather anasema "pale watu wanaposimama kudai haki zao na kutaka mazingira yao yalindwe, wananyamazishwa kikatili".