TANZANIA-NZIGE-FAO

Tanzania kutumia ndege kuangamiza nzige

Nzige katika eneo la Nanyuki nchini Kenya
Nzige katika eneo la Nanyuki nchini Kenya REUTERS/Baz Ratner

Serikali ya Tanzania inapania kutumia ndege mbili ndogo, kukabili nzige ambao wamevamia maeneo ya Longido, Simanjiro na Manyara, amesema waziri wa kilimo, Adolf Mkenda.

Matangazo ya kibiashara

Mkenda, tayari imezuru maeneo husika na kuahidi msaada wa serikali kudhibiti nzige hao ambao tayari wamesababisha hasara kwa baadhi ya wakulima.

Waziri Mkenda ameongeza ndege moja ya shirika la mpango wa chakula ya Umoja wa mataifa (FAO), imeagizwa kutoka nchini kenya, ili kusaidia katika kuwanyunyuzia nzige hao dawa.

Hata hivyo waziri Mkenda, imepuuza tetesi kuwa huenda nzige hao wakasabisha hasara kubwa kwa wakulima, akisema wapo katika hali ya kuzaliwa kwa hivyo zoezi la kuwanyunyuzia dawa litakapokamilika basi  hawataonekana tena.

Zoezi la kuwanyunyuzia dawa linatarajiwa kuchukuwa kipindi cha siku tatu.

Nzige wamevamia mataiafa kadhaa ya Afrika yashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Somalia na Ethiopia.