Mchakato wa uteuzi wa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki mashakani

Katibu mkuu wa jumuia ya Afrika mashariki Liberat Mfumukeko wakati wa mkutano na waandishi wa habari Oktoba 2016-EAC Secretariat
Katibu mkuu wa jumuia ya Afrika mashariki Liberat Mfumukeko wakati wa mkutano na waandishi wa habari Oktoba 2016-EAC Secretariat ©

Mchakato wa mataifa wanachama kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki kujaza nafasi ya katibu mkuu  wa jumuiya ya Afika mashariki, Liberat Mfumukeko anayemaliza muhula wake mwezi Aprili unazidi kuibua hisia kali ambapo mataifa wanachama yanaendelea kuvutana kuelekea kukamilika mchakato huo.

Matangazo ya kibiashara

Hali hii imejitokeza baada ya Kenya na Sudan Kusini, kutangaza azma ya kuteua mwaniaji kwenye nafasi hiyo.

Kwa kawaida nafasi hiyo huwa ni ya kupokezana kati ya mataifa wanachama na japo zamu ya Kenya kujaza nafasi hiyo ,Sudan Kusini ,taifa la hivi majuzi kujiunga na jumuiya limetangaza lipo kwenye kinyanganyiro hicho.

Hii ni licha ya  Sudan Kusini kutuhumiwa kuwa na deni kubwa la  ada ya uanachama na  bado haijapitisha sheria  hitajika za kuwezesha biashara huru na umoja wa forodha.

Wanaotazamiwa kuwania kiti hicho kutoka Kenya ni katibu mtendaji katika wizara ya mambo ya nje Ababu Namwamba, Waziri wa ustawi wa jumuiya ya Afrika Mashariki Aden Mohammed  na waziri wa michezo Amina Mohammed.

Sudan Kusini kwa upande wake ,imempendekeza aliyekuwa waziri wa fedha Aggrey Tisa Sabuni