UGANDA-SIASA-USALAMA

Uganda yaitaka Marekani kutoingilia masuala yake ya ndani

Yoweri Museveni aliingia madarakani mnamo 1986 kupitia mapinduzi ya kijeshi .
Yoweri Museveni aliingia madarakani mnamo 1986 kupitia mapinduzi ya kijeshi . © AFP - Sumy Sadurni

Uganda imeshtumu Marekani, baada ya nchi hiyo kuishtumu kuhusu kwa kuwahangaisha wapinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Januari.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Ofwono Opondo, amesema, Marekani inastahili kushughulikia matatizo yake ya uchaguzi badala ya kuishauri na kuitisha Uganda.

Kauli hii ya Uganda imekuja baada ya Wizara ya mambo ya nje ya Marekani kutangaza kuwa inalenga kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wa Uganda hasa maafisa wa usalama kuhusiana na uchaguzi wa Jnauari ambao upinzani umekuwa ukidai kuwa uliibiwa.

Mpinzani mkuu rais Museveni, Bobi Wine alisema uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu mkubwa na kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi huo mahakamani kabla ya kuoindoa>

Tume ya Uchaguzi ikiungwa mkono na Mahakama ya Katiba ilimtangaza Yoweri Museveni mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia 59 ya kura dhidi ya mpizani wake Bobi Wine aliyepata asilimia 35 ya kura.