KENYA - SIASA

Naibu rais wa Kenya hatapinga mchakato wa kufanyia katiba marekebisho

Naibu rais wa Kenyan  William Ruto
Naibu rais wa Kenyan William Ruto file.jpg

Naibu rais wa Kenya, Willam Ruto, amedokeza uwezekano wake wa kutopinga kura ya maoni inayolenga kufanyia marekebisho katiba ya taifa hilo, maaarufu kama Building Bridges Initiative (BBI) .

Matangazo ya kibiashara

Ruto ambaye wengi walitarajia kuwa angepinga mchakato huo, baada kuibua tetesi kuhusiana na vipengee kadhaa alivyodai kuwa tata, amesema wakenya wanastahili kupewa nafasi, kupinga au kukubali BBI, na wala si kulazimishwa kupitisha marekebisho hayo.

Kuna wengine wanatarajia ati mimi nitaongoza mrengo huu au mrengo ule, mimi ni mtu ambaye anaaminia demokrasia…ile itaamuliwa na wakenya niko tayari kutumia…kama ni katiba ya sasa au katiba itakayokuja, niko tayari,

amesema Ruto.

Aidha amekosa hatua ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wanawao shinikiza marekebisho hayo, kwa kutumia maafisa wa usalama kuwatisha wanaopinga marekebisho ya katiba, pamoja na kutumia pesa kuwahonga baadhi ya viongozi kuunga mkono BBI.

Mabunge ya kaunti 42 kati ya 47 nchini Kenya tayari yamepitisha mswada wa wa BBI, na sasa unatarajiwa kuwalishwa kwa bunge la kitaifa na seneti, kabla ya kufikishwa kwa raia kuukataa au kuukubali.

Yaliomo ndani ya BBI

Iwapo marekebisho hayo yatapita, taifa la Kenya mbali na kuwa na rais na naibu wake  litakuwa na waziri mkuu pamoja na manaibu wake wawili pamoja na maeneo bunge 70 kuongezwa kwa ya sasa 290.

 Kadhalika pesa zinazotolewa na serikali kuu kwa serikali za kaunti zinatarajiwa kuongezwa kutoka asilimia 15 hadi 35 ili kufadhili zaidi miradi ya maendeleo mashinani.

Rais Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga wanatarajiwa kuanza kuongoza kampeini za kupigia upato marekebisho hayo ya katiba kuanzia jumatatu juma lijalo, kura ya maoni ikitarajiwa mwezi juni, kwa mjibu wa Odinga.