JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI - MAENDELEO

Rais wa Kenya ateuliwa mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika mashariki

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliposhiriki mkutano wa jumuiya Afrika mashariki pitia njia ya Video. 27 02 2021
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliposhiriki mkutano wa jumuiya Afrika mashariki pitia njia ya Video. 27 02 2021 Presidential Press Service/Handout via Reuters

Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamekutana katika kikao kupitia mtandao kutokana na janga la corona.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka nchi wanachama kuungana kutatua changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo, kama kuwepo kwa janga la Corona na kuwawezesha wananchi katika Jumuiya hiyo kutangamana bila ya kuwepo kwa masharti.

Rais kenyatta amesema kuna umuhimu wa nchi wanachama kutekeleza kwa vitendo, makubaliano ya watu kutembea na kufanya biashara   kwa watu na wafanyikazi bila ya vikwazo kama ilivyo kwenye mkataba, amesema Kenya imekubali watu kutoka kwenye jumuiya  kufanya baishara, na kujihusisha katika mambo mengine ya kijamlii bila ya vikwazo vyovyote.

 Katika hatua nyingine, marais wa Jumuiya hiyo wamemtea Peter Mathuki kutoka nchini Kenya, kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo kwa miaka mitano ijayo na anachukua nafasi ya Liberat Mfumukeko kutoka Burundi anayemaliza muda wake mwezi Aprili.

Kikao cha leo kimehudhuriwa na marais wa kutoka mataifa yate ya kujumuiya hiyo, huku makomu rais wa Tanzania Samia Suluhu akimwakilisha rais John Magufuli.