TANZANIA-KANISA KATOLIKI-CORONA

Kanisa Katoliki nchini Tanzania lahimiza tena tahadhari dhidi ya maambukizi ya Corona

Baadhi ya waumini wa dini ya Kikiristo nchini Tanzania, rais wa nchi hiyo John Magufuli amekuwa akiwaambia raia wa nchi hiyo kumwomba Mungu kushinda janga la Corona.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikiristo nchini Tanzania, rais wa nchi hiyo John Magufuli amekuwa akiwaambia raia wa nchi hiyo kumwomba Mungu kushinda janga la Corona. © AFP - STRINGER

Kanisa Katoliki nchini Tanzania kwa mara nyingine, linataka raia wa nchi hiyo kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya janga la Corona, baada ya Mapadri 25 na Masista zaidi ya 60 kufariki dunia kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita baada ya kupata changamoto ya upumuaji, zinazohusishwa na virusi vya corona.

Matangazo ya kibiashara

Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa hilo, akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano, amesema tishio la Corona bado lipo nchini humo, na linadhihirishwa na idadi ya vifo inayoendelea kushuhudiwa hata ndani ya Kanisa hilo.

Ndani ya miezi iliyopita Mapadri 25 wamepoteza maisha kwa matatizo ya kupumua huku  Masisita na manesi zaidi ya 60 não pia wakipoteza maisha, hii sio hali ya kawaida tuchukue tahadhari.

Aidha, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania amesema japo Wiazara ya afya nchini humo imekuwa ikitoa tahadhari kwa watu kuchukua tahadhari, hakuna sheria inayowalazimu watu kufanya hivyo na hivyo ni vigumu wananchi wengi wa kawaida kuchukulia suala hili kwa umakini.

Rais John Magufuli ambaye hajaweka wazi iwapo nchi hiyo ina Corona, amekuwa akiwaaambia raia wake waendelee kuomba na kumtegemea Mwenyezi Mungu, lakini Kitima amesema kumwomba pekee hakuwezi kuondoa tatizo hilo nchini humo.

 Mungu si hirizi, anataka binadamu tuwajibike. Corona ipo, unaambiwa chukua tahadhari unasema ushasali...Mungu wetu anataka tuwajibike , tutende majukumu yetu kwa karama na utashi tuliopewa.

Tahadhari hii ya Kanisa katoliki imekuja baada ya  Shirika la afya duniani (WHO), kutaka Tanzania kuchukua hatua zaidi kukabiliana na Covid-19.