KENYA - SIASA

Mtikisiko ndani ya chama tawala nchini Kenya

Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta  akiwa katika makao makuu ya chama tawala cha Jubilee jijini  Nairobi.
Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta akiwa katika makao makuu ya chama tawala cha Jubilee jijini Nairobi. REUTERS/Baz Ratner

Chama tawala nchini Kenya Jubilee kinaendelea kupata mtikisiko, baada ya uongozi wa chama hicho kumwondoa katika nafasi yake, naibu katibu mkuu Caleb Kositany kwa tuhuma za ukiukaji wa maadili.Mwanahabari  Benson Wakoli amezungumza na naibu katibu mkuu huyo wa zamani akiwa jijini Nairobi nchini kenya.