KENYA-AFYA-UCHUMI

COVID-19: Kampeni ya kutoa chanjo kwa raia yaanza Kenya

SMamlaka nchini Kenya ikipokea chanjo ya kwanza dhidi ya COVID-19 huko Nairobi.
SMamlaka nchini Kenya ikipokea chanjo ya kwanza dhidi ya COVID-19 huko Nairobi. TONY KARUMBA AFP

Kenya imezindua kampeni ya kutoa chanjo kwa watu nchini humo dhidi ya virusi vya Covid-19 wakati visa vya maambukizi vikiendelea kuripotiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Kampeni hiyo imezinduliwa katika Hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi, na watu wa kwanza kupata chanjo hiyo aina ya AstraZeneca ni wahudumu wa afya.

Maafisa wa juu kutoka Wizara ya afya, nao wamepokea chanjo hiyo kuonesha kuwa iko salama, siku moja baada ya Madaktari wa Kanisa Katoliki kuwataka raia wa nchi hiyo kupuuza chanjo hiyo.

Wiki hii, Kenya ilipokea chanjo zaidi ya Milioni moja kutoka kwa kampuni ya Astrazeneca na ifikapo mwewni Juni, watu zaidi ya Milioni Moja na Laki Mbili wanatarajiwa kupàata chanjo hiyo;