Kenya

Kenya: Wazee wa kabila la Samburu wapinga dhidi ya ukeketaji

Mwanamke wa kabila la Pokot nchini Kenya wakati wa hafla ya ukeketaji Oktoba 16.
Mwanamke wa kabila la Pokot nchini Kenya wakati wa hafla ya ukeketaji Oktoba 16. REUTERS/Siegfried Modola

Nchini Kenya, Machi 5, wazee 40 kutoka vijiji vya kaskazini mwa Kaunti ya Samburu walitangaza hadharani kwamba wamejitolea kusitisha ukeketaji na ndoa za utotoni.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe·hiyo·iliongozwa·na·rais·Uhuru·Kenyatta·ambaye·alisema·atahakikisha·vitendo·vinakomeshwa·nchini·Kenya.

Hili·ni·"tamko·la·kihistoria",·kulingana·na·mashirika·yanayopambana·na·ukeketaji,·na·"hatua·muhimu"·kwa·haki·za·wasichana,·kulingana·na·rais·wa·Kenya·Uhuru·Kenyatta,·ambaye·alisema·ni·moja·ya·mambo·anayopambana·nayo.·Mnamo·mwaka·wa·2019,·alitangaza·wazi·nia·yake·ya·kuona·ukeketaji·unakomeshwa·nchini·kufikia·mwaka·2022.

Kenya·yapiga·marufu·ukeketaji

Tamko·la·wazee·wa·vijiji·vya·Samburu,·hata·hivyo,·linakuja·wakati·ambapo·ukeketaji·ulikuwa·tayari·umepigwa·marufuku·nchini·Kenya·tangu·mwaka·2011.·Lakini·vitendo·hivyo·bado·vinaripotiwa·katika·baadhi·ya·jamii.·Katika·ngazi·ya·kitaifa,·21%·ya·wanawake·wenye·umri·kati·ya·miaka·15·na·49·tayari·wamefanyiwa·ukeketaji,·kwa·mujibu·wa·Shirika·la·Umoja·wa·Mataifa·la·kuhudumia·watoto·UNICEF.

Wasichana·wengi·hukatiziwa·elimu·kwa·kuozwa·baada·ya·kukeketwa.·Ukeketaji·umekithiri·katika·kaunti·za·Pokot·Magharibi·na·Tana·River

Hivi·karibuni·viongozi·wa·dunia·waliahidi·kutokomeza·ukeketaji·ifikapo·mwaka·2030,·lakini·wanaharakati·wanasema·utamaduni·huo·hatari·na␣·uliopitwa·na·wakati·bado·umekita·mizizi·katika·maeneo·mengi.Kulingana·na·takwimu·za·shirika·la·Umoja·wa·Mataifa·linalowahudumia·watoto·UNICEF,·ukeketaji·unafanyika·katika·mataifa·yasiyopungua·30,·mengi·yakiwa·ya·Afrika,·Mashariki·ya·Kati·na·Asia.

Ukeketaji·ni·nini

Ukeketaji·unamaanisha·baadhi·ya·viungo·vya·sehemu·za·siri·za·msichana·au·mwanamke·ama·zinakatwa·kwa·sehemu·fulani·au·zinanyofolewa·kabisa.·Katika·baadhi·ya·makabila·huwa·wanashona·sehemu·hizo·au·kuzichanja.

Ukeketaji·unaweza·kusababisha·matatizo·ya·muda·mrefu·ya·kiafya·na·kisaikolojia,·ikiwemo·maambukizi·ya·mara·kwa·mara·ya·maeneo·ya·siri,·kupata·matatizo·wakati·wa·hedhi,·kukosa·kuzaa·na·matatizo·wakati·wa·kujifunga.

Kumekuwa·na·ongezeko·la·mtindo·wa·wahudumu·wa·afya·kufanya·ukeketaji·badala·ya·mangariba·wa·kimila·hasa·Misri,·Guinea,·Kenya,·Nigeria·na·Sudan.·Sababu·kubwa·inayotolewa·ya·kuwakeketa·wasichana·huwa·ni·kujaribu·kudhibiti·hamu·ya·ngono.

Finland·itaahirisha·uchaguzi·wake·wa·sewrikali·za·mitaa·uliopangwa·kufanyika·mwezi·ujao·hadi·katikati·ya·mwezi·Juni.·Kuongezeka·kwa·visa·vya·maambukizi·ya·virusi·vya·Corona·kumezidisha·hofu·ya·uwezekano·wa·maambukizi·zaidi·baada·ya·uchaguzi·huo,·Waziri·wa·Sheria·ametangaza.