Burundi - Kilimo

Burundi yapiga marufuku uingizwaji wa mahindi kutoka nje ya nchi

Mahindi
Mahindi Ronaldo Schemidt AFP/File

Wizara ya biashara nchini Burundi imepiga marufuku uagizaji wa mahindi na unga kutoka mataifa  ya kigeni kwa muda wa miezi sita zijazo kuanzia Machi 8 mwaka 2021.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka wizara hiyo imesema imegundulika kuwa mahindi yanayoagizwa kutoka nje ya nchi hiyo si salama na yanaweza kuathiri afya za watu katika taifa hilo la Afrika ya Kati.

Hata hivyo, Burundi haijaweka wazi ni mataifa yepi hayo iliyozuia kuingiza mahindi nchini humo, lakini mara nyingi nchi hiyo huagiza mahindi kutoka mataifa ya Uganda na Zambia.

Hatua hii ya Burundi inakuja baada ya juma lililopita, Kenya kupiga marufuku mahindi kutoka nchi jirani za Tanzania na Uganda, kwa kile ilichosema, yalikuwa na sumu na hivyo hatari kwa matumizi ya binadamu.

Kuna idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaotumia mahindi kama chakula chao kikuu.

I