TANZANIA-MAGUFULI

Rais Magufuli yuko wapi ? Wapinzani nchini Tanzania wauliza

Picha ya maktaba ya rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Picha ya maktaba ya rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Thomas Mukoya/File Photo

Wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, wanashikiza kufahamuu aliko rais wa nchi hiyo John Magufuli ambaye hajaonekana hadharani kwa wiki mbili sasa, hatua ambayo imezua maswali kuhusu afya yake.

Matangazo ya kibiashara

Kutoonekana kwa rais huyo, kumezua uvumi kwenye mitandao ya kijamii, huku ikihofiwa kuwa huenda anasumbuliwa na mamabukizi ya Covud 19.

Mara ya mwisho kwa Magufuli kuonekana hadharani ilikuwa ni Februari 27 wakati akimwapisha Katibu Mkuu kiongozi na hata hakuonekana wakati wa kikao cha viongozi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichofanyoka kupitia njia ya mtandao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mwanasiasa wa upinzani Tundu Lissu ambaye aligombea urais mwaka 202O aliandika siku ya Jumanne kuwa, umma wa Tanzania unastahili kufahamu aliko kiongozi wao.

 

Gazeti la nchi jirani ya Kenya, Daily Nation, liliandika siku ya Jumatano kuwa kiongozi mmoja kutoka taifa la Afrika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Nairobi.

Afisa katika Hospitali ya Nairobi alipoulizwa na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, iwapo kiongozi aliyelazwa ni rais Magufuli, alisema hana taarifa hizo, lakini pia vyanzo katika serikali ya Kenya vimesema havina taarufa yoyote.

Naye Katibu Mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalendo Ado Shaibu, ameiambia AFP kuwa pamoja na kwamna suala la afya ya mtu ni kitu binafsi, kwa kiongozi mkubwa ni muhimu umaa uelewze kinachoendelea.

Serikali ya Tanzania haijasema chochote kuhusu ni wapi aliko rais Magufuli, lakini siku ya Jumatano, Waziri wa Habari Innocent Bashungwa aliwaonya wananchi na vyombo vya Habari kuacha kutumia uvumi kama chanzo chao cha habari.