Watu zaidi ya 200,000 wapokea chanjo ya Corona nchini Rwanda
Imechapishwa:
Raia wa Rwanda wapatao 228,854 tayari wamepokea chanjo ya kuzuia maambukizi ya Covid 19, wiki moja baada ya kuanza kutolewa nchini humo.
Miongoni mwa watu wa kwanza wanaopokea chanjo hiyo ni pamoja na wahudumu wa afya, Walimu na wazee wenye zaidi ya miaka 65, wanaosumbuliwa na magonjwa hatarishi.
Watu wengine wanaoendelea kupokea chanjo ni pamoja na wafungwa, madereva taxi na wakimbizi wanaoishi nchini humo miongoni mwa wengine.
Awali, Rwanda ilikuwa imepanga kuwapa chanjo watu 171,480 katika awamu ya kwanza ya utoaji wa chanjo hiyo.
Tarehe 3 na 4 mwezi Machi, Rwanda ilipokea chanjo 340,960 kutoka kampuni ya AstraZeneca na Pfizer huku ikipata dozi nyingine 50,000 kutoka India, waliopewa kama msaada.