KENYA-COVID 19

Kenya yapiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa siku 30 kudhibiti Covid 19

Le président kenyan Uhuru Kenyatta dans un discours enregistré pour l'ONU, le 3 décembre 2020.
Le président kenyan Uhuru Kenyatta dans un discours enregistré pour l'ONU, le 3 décembre 2020. AP

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta siku ya Ijumaa, ametangaza kupiga marufuku mikutano ya kisiasa na mikusanyiko mikubwa ya watu kwa siku 30 baada ya nchi hiyo kuanza kushuhudia ongezeko la maambukizi ya Covid 19.

Matangazo ya kibiashara

Kenyatta amewataka maafisa wa usalama kuhakikisha kuwa, marufuku hayo yanatekelezwa kikamilifu huku akionya kuwa yeyote atakaye kwenda kinyume, atakamatwa na kufungiliwa mashtaka.

Wiki hi,i Kenya iliripoti maambukizi makubwa zaidi ya maambukizi ya Corona ambayo ni zaidi ya 800, na kuzua hali ya wasiwasi nchini humo baada ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuanza kushuhudia kushuka kwa maambukizi hayo mwezi Januari.

Marufuku ya watu kutotembea nje ambayo yamekuwa yakiendelea nchini humo tangu mwaka 2020, yataendelea kwa siku zingine 60 kati ya saa nne usiku mpaka saa 10 Alfajiri.

Mazishi yatatakiwa kufanyika na kumalizika baada ya saa 72 ya mtu kupoteza maisha, na watakaohudhuria ni familia ya marehemu  na idadi ya waombolezaji  isizidi 100.

Sherehe za harusi zitaendelea lakini watu watakaohudhuria hawatazidi 100.

Masharti haya mapya yamekuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea na mpango wa kutoa chanjo kwa raia wake.

Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga, amekuwa kiongozi wa juu kuambukizwa virusi hivyo.

Kenya ina maambukizi ya Corona, zaidi ya 111,000 na watu wengine zaidi ya 1,900 wamepoteza maisha tangu mwezi Machi mwaka 2020.