KENYA-ODINGA-COVID 19

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aambukizwa Covid 19

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, ajiondoa kwenye marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 26 2017.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, ajiondoa kwenye marudio ya uchaguzi wa urais Oktoba 26 2017. AFP/File

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ameambukizwa virusi vya Covid 19 lakini madaktari wake wanasema hali yake inaimarika wakati huu akiwa amelazwa hospitalini jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Kuambukizwa kwa Odinga, kunakuja wakati huu watu wengine 829 wakiambukizwa siku ya Alhamisi na tayari Waziri wa afya Mutahi Kagwe amesema nchi hiyo inashuhudia mlipuko wa tatu wa maambukizi hayo.

Kiongozi wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta anatarajiwa kulihotubia taifa siku ya Ijumaa, kuhusu mapambano dhidi ya maambukizi hayo ambayo yamewaambukiza watu zaidi ya 111,000  kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Kenya tayari inaendelea na mchakato wa kutoa chanjo kwa makundi ya watu mbalimbali  nchini humo wakiwemo wahudumu wa afya baada ya kupokea chanjo zaidi ya Milioni Moja, aina ya AstraZeneca wiki iliyopita.

Siku ya Alhamisi, Kenya ilipokea msaada wa chanjo nyingine 100,000 aina ya AstraZeneca kutoka nchini India.

Watalaam wa afya katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa Afrika Mashariki, wameendelea kutoa wito kwa watu nchini humo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi hayo, kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotitirika na kukaa umbali wa aungalau Mita moja.