TANZANIA

Tanzania yaomboleza kifo cha rais Magufuli

John Pombe Magufuli, rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano Machi 17, 2021.
John Pombe Magufuli, rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano Machi 17, 2021. Ikulu/Tanzania

Serikali ya Tanzania imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 14 baada ya rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli kuaga dunia Jumatano majira ya saa 12:00 jioni kutokana na tatizo la moyo.

Matangazo ya kibiashara

John Magufuli, rais mzalendo mwenye kauli za kupinga masharti ya kudhibiti janga la Corona, hajaonekana hadharani tangu mwishoni mwa mwezi Februari.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salaam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.

Rais Magufuli alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa hawaamini uwepo wa ugonjwa wa COVID-19.

Mwaka uliopita alisema Tanzania ilifanikiwa kupambana na kuudhibiti ugonjwa huo kupitia siku tatu za maombi.

Tangazo la kifo chake linajiri zaidi ya wiki mbili tangu alipoonekana hadharani na kuzua uvumi kwamba alikuwa akiugua virusi vya Corona.