TANZANIA

Tanzania: Ratiba ya mazishi ya kitaifa ya Magufuli kutolewa leo

Rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano hii, Machi 17, akiwa na umri wa miaka 61, kutokana na matatizo ya moyo.
Rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano hii, Machi 17, akiwa na umri wa miaka 61, kutokana na matatizo ya moyo. AFP

Ratiba ya mazishi ya hayati rais John Pombe Joseph Magufuli inatarajiwa kutangazwa leo Ijumaa na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ataapishwa kuwa rais wa sita Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Tanzania, Dk Hassan Abbas ameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba, utaratibu wa maizishi yake na ratiba ya maziko utatolewa asubuhi hii na Makamu wa Rais wa Tanzania,Bi Samia Suluhu

Jeneza la Magufulilitapitishwa ili kutazamwa na wananchi katika barabara kuu, kulingana na msemaji wa Serikali Hassan Abbas.

Raia wataweza kuuona mwili wa Magufuli katika miji ya Dar es salaam, Dodoma, Mwanza na Chato, mji anakotoka hayati rais Magufuli.

Makamu wa rais, Samia Suluhu. Anatarajia kulihutubia taifa leo asubuhi na kuratibu mipango mingine kabla ya mazishi ya Magufuli amesema Hassan Abbas.

Rais wa Tanzania aliaga dunia Jumatano hii, Machi 17, akiwa na umri wa miaka 61, kutokana na matatizo ya moyo