Tanzania - Siasa

Tanzania ni salama mikononi mwa Suluhu, aseme Kikwete

Rais wa  Tanzania, Samia Suluhu Hassan, baada ya kuapishwa 19 machi 2021.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, baada ya kuapishwa 19 machi 2021. REUTERS - STRINGER

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema taifa la Tanzania liko salama chini ya uongozi wa rais mpya Samia Suluh, kwani rais huyo anafahamu kile kimetendeka Tanzania, kinachostahili kufanyika na mipango ya serikali miaka tano ijayo;

Matangazo ya kibiashara

Kikwete amewataka watanzania kushirikiana na rais Suluhu, kufutia kifo cha ghafla cha rais John Pombe Joseph Magufuli, akisema yeyé binafsi hakutarajia kifo hicho na kwamba uongozi wake ulipendwa sana na watazania.

Kikwete kupitia mtandao wake wa twitta amesema Magufuli alitakiwa kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoanza,ila kukatokea msiba ambao watanzania wanazidi kuomboleza.

Amesema ana imani na rais Suluhu kwani amekuwa makomo rais Tangu mwaka 2015, walipochukuwa serikali chini ya chama cha CCM.

Mipango ya Mungu

Kikwete amesema raia wengi wa taifa hilo walitamani Magufuli kutawala Tanzania kwa kipindi kirefu, ila mipango ya Mungu haiwezi kusolewa.

Letu sisi ni kumuombea Mungu ndugu yetu alale kwa amani 

amesema Kikwete, akisisitiza kuwa taifa litamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoyafanya, akimtaja hayati Magufuli kuwa, jasiri, mzalendo na mwenye mipango aliyotekeleza.

 

Ujumbe wa rais Mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete