TANZANIA

Zanzibar yaaga mwili wa hayati rais Magufuli

Maafisa wa jeshi wakisindikiza magari yanayobebea mwili wa hayati rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Maafisa wa jeshi wakisindikiza magari yanayobebea mwili wa hayati rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS - STRINGER

Wakaazi wa Zanzibar leo wanaaga mwili wa rais hayati John Pombe Joseph Magufuli ambaye atazikwa siku ya Ijumaa nyumbani kwao huko Chato.

Matangazo ya kibiashara

Jumatatu wiki hii kulikuwa na msiba wa kitaifa mjini Dodoma uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mataifa ya Afrika, na akizungumza katika msiba huo, rais Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine amewahakikishia Watanzania kuwa nchi hiyo itakuwa salama chini utawala wake.

Watanzania wanapoendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa kiongozi wao John Magufuli, familia moja jijini Dar Es Salaam imepoteza watu watano baada ya kutokea kwa mkanyagano mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wakaazi wa jiji hilo walipojitokeza kuuga mwili wa kiongozi huyo.

Dennis Mtuwa amepoteza mke wake, watoto  wake wawili, na wapwa zake wawili waliokuwa wamekwenda katika uwanja wa Uhuru. Ripoti ambazo hazijathibitishwa, zinasema kuwa watu zaidi ya 40 walipoteza maisha katika mkanyagano huo.