UGANDA

Wanne wakamatwa kwa kuuwa Simba sita Uganda

Waliokamatwa ni raia wa Uganda, huku mdogo akiwa na umri wa miaka 26 wakati mkubwa ana umri wa miaka 68.
Waliokamatwa ni raia wa Uganda, huku mdogo akiwa na umri wa miaka 26 wakati mkubwa ana umri wa miaka 68. Reuters/James Akena

Polisi nchini Uganda, wamewakamata watu wanne, wanaohusishwa na madai ya kuwauwa Simba sita, katika hifadhi ya taifa ya Queen Elizabeth kwa kuwapa sumu.

Matangazo ya kibiashara

Watu wanne wamekamatwa kwa kuhusishwa na kuua simba sita adimu wanaopanda miti katika Hifadhi ya Queen Elizabeth nchini Uganda 

Kuuawa kwa simba hawa wiki iliyopita kulisababisha mamlaka inayoshugulikia wayama pori (Wild Life Authority ) kutoa zawadi ya shilingi milioni kumi za Uganda kwa mtu yeyote ambaye angeweza kutoa habari inayosababisha washukiwa kukamatwa.

 Waliokamatwa ni raia wa Uganda, huku mdogo akiwa na umri wa miaka 26 wakati mkubwa ana umri wa miaka 68.

“Tulipata habari kutoka kwa mtu ambeye alitusaidia akasema wacha niwasaidie niwape habari inayoweza kusaidia kuwakamata watu hawa. Tulipofuatilia hii habari tuliweza kufanya oparesheni. Baada ya watu hawa kukamatwa, tuliwakuta na vichwa vinne vya simba, vitatu vilikua vimefichwa kwenye mtii halafu kichwa cha inne walikua wamekizika na miguu kumi na tano. Wanasheria watatuelekeza kuhusiana na mashitaka ambayo tutawasilisha mahakamani”, amesemaBashir Hangi, msemaji wa Mamlaka inayoshugulikia nyama za pori hapa Uganda-Uganda Wild Life Authority

 Kwa mujibu wa sheria nchini Uganda, adhabu ya juu kabisa ambayo mtu anaweza kupewa baada ya kupatikana kuwa ameua wanyama pori waliolindwa ni shilingi bilioni 20 za Uganda, kifungo cha maisha, au hukumu zote mbili.

Utalii ni sekta ambayo inaiingizia Uganda kipato kikubwa na kabla ya jangwa la COVID-19 sekta hii ilikuwa ikichangiya karibu dola bilioni 1.4 kila mwaka. Kuuawa kwa wanyama pori kama simba ni tishio kubwa kwa sekta ya utalii nchini Uganda.