TANZANIA

Hayati magufuli kuzikwa kwenye makaburi ya familia Chato

Rais Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam tarehe 17 Machi.
Rais Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam tarehe 17 Machi. REUTERS - STRINGER

Mwili wa hayati John Pombe Magufuli hii leo Ijumaa utazikwa katika makaburi ya familia huko mjini Chato, mkoani Geita, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya wananchi tayari wameanza kujitokeza katika uwanja wa Magufuli ambapo kutakuwa na misa maalumu kabla ya mazishi.

Mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli utapelekwa kanisani kwa ibada maalumu.

Rais Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam tarehe 17 Machi

Magufuli ni rais wa kwanza nchini Tanzania kufariki akiwa madarakani na hatua hiyo inalifanya taifa hilo kuongozwa na rais mwanamke kwa mara ya kwanza, Rais Samia Suluhu Hassan.