TANZANIA

Rais wa Tanzania amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari

Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania.
Samia Suluhu Hassan, rais wa Tanzania. AP

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini humo TPA Deusdedit Kakoko, kupisha uchunguzi wa ubadhirifu wa fedha bandarini.

Matangazo ya kibiashara

Rais Samia ametoa kauli hii hivi leo baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Takukuru Ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Ripoti nimeona, nimeipitia na nimebaini ubadhirifu mkubwa uliofanywa pale bandari, hili suala mnatakiwa kushirikiana, nakuomba Takukuru jishughulishe pale, alipita Waziri Mkuu alilishughulikia.
Waziri Mkuu aliunda kamati na wakafanya uchunguzi kidogo ambao yaliyotoka, hatua chache zilichukuliwa lakini imani yangu ni kwamba kama kuna ubadhirifu pale waliosimamishwa ni hawa wa chini huku, ninaomba mara moja nitoe agizo la kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa Bandari halafu hatua zaidi ziendelee,

 

Haya ndio maamuzi ya kwanza kuchukuliwa na rais huyo mpya wa Tanzania, baada ya kufariki kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Magufuli.