BURUNDI

Washington yashtumu Burundi kwa ukiukwaji wa haki za binadamu

Uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza ni moja wapo ya haki za binadamu zinazokiukwa mara kwa mara nchini Burundi, inasema ripoti kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza ni moja wapo ya haki za binadamu zinazokiukwa mara kwa mara nchini Burundi, inasema ripoti kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. AFP/ Esdras Ndikumana

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imechapisha ripoti  yenye kurasa 40 kuhusu Burundi inaonyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ambao unaendelea licha ya mabadiliko ya uongozi.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imekusanya ripoti kadhaa kutoka kwa mashirika ya kiraia ya ndani na ya kimataifa na matokeo ya Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa.

Moja ya mambo chanya yaliomo kwenye ripoti hiyo ni makabidhiano ya uongozi yaliofanyika kwa amani licha ya uchaguzi kugubikwa na kasoro chungu nzima.

Kwa mengine yote yaliosalia, matokeo yake ni hasi. Ripoti hiyo kwanza imechambua hali mbaya iliopo katika magereza nchini Burundi. Sehemu zilizojaa watu: magereza rasmi 13 ambayo yana uwezo wa wafungwa karibu 4,200 na badala yake yanapokea idadi mara tatu ya hiyo. Hakuna maji, vyoo au umeme, wafungwa wengi hufa kwa magonjwa.

Polisi na Imbonerakure wahusishwa katika ukatili Burundi

Uchunguzi mwingine ni kwamba tangu uchaguzi wa 2020, ukiukaji wa haki za binadamu haujakoma, mbali nayo. Wahusika wakuu ni vikosi vya polisi, lakini pia wanachama wa tawi la Vijana wa chama kilicho madarakani ambao wanaendelea kufurahiya hali iliopo ya kutoadhibu.

Aidha Kuhusu mauaji ya watu wanaopoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyoimbo vya usalama yameendelea kuripotiwa ambapo watu  zaidi 200 waliorodheshwa mwaka jana. Vivyo hivyo kwa kukamatwa kiholela, utekaji nyara na mateso ya wapinzani au watu binafsi wanaodhaniwa kuwa wapinzani.

Mwishowe, katika ripoti hiypo mbaya kwa Burundi inaonyesha pia vizuizi juu ya uhuru wa kujieleza na inaonyesha kukamatwa kwa waandishi wa habari bila sababu