UFARANSA

Ripoti ya Duclert: Ufaransa na Rwanda zapiga hatua muhimu

Mwanahistoria Vincent Duclert akimkabidhi rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ripoti ya tume iliopewa kazi ya kuchunguza jukumu la Ufaransa katika mauaji ya Kimbari ya Rwanda.
Mwanahistoria Vincent Duclert akimkabidhi rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ripoti ya tume iliopewa kazi ya kuchunguza jukumu la Ufaransa katika mauaji ya Kimbari ya Rwanda. AFP - LUDOVIC MARIN

Rwanda inaanza maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Matangazo ya kibiashara

Haya ni maadhimisho ya 27 tangu kutokea kwa mauaji hayo. Inakadiriwa watu milioni moja waliuawa kwa kipindi cha siku 100.

Maadhimisho ya kipekee nchini Ufaransa: siku kumi na mbili zilizopita, tume ya Duclert ilimkabidhi rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ripoti yake juu ya jukumu la Ufaransa wakati na kabla ya mauaji ya halaiki.

Hata hivyo tume hiyo iliopewa kazi ya kuchunguza jukumu la Ufaransa katika mauaji ya Kimbari ya Rwanda, haikubainisha uungwaji mkono wa Ufaransa katika mauaji ya Kimbari lakini imesema Ufaransa ilikuwa na jukumu kubwa katika mauaji hayo.

Ripoti hiyo inaashiria hatua muhimu ya kurejea kwa uhusiano wa Rwanda na Ufaransa ambapo kuna uwezekano mkubwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akafanya ziara jijini Kigali mwezi ujao.