KENYA

Wakenya wataka kuwepo na uwazi zaidi juu ya matumizi ya mikopo ya IMF

Mfuko maalum kutoka IMF unaweza kutengwa kwa nchi zilizoendelea zaidi, kuzisaidia kukabiliana na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na janga la Covid-19. Hapa, nembo ya taasisi hiyo kwenye makao makuu yake huko Washington, Septemba 4, 2018.
Mfuko maalum kutoka IMF unaweza kutengwa kwa nchi zilizoendelea zaidi, kuzisaidia kukabiliana na mgogoro wa kiafya unaosababishwa na janga la Covid-19. Hapa, nembo ya taasisi hiyo kwenye makao makuu yake huko Washington, Septemba 4, 2018. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo

Fedha zilizotolewa na shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, kwa minajili ya kupambana dhidi ya janga la Covid-19 zimezua sintofahamu nchini Kenya.

Matangazo ya kibiashara

IMF iliidhinisha Aprili 2 msaada wa dola bilioni 2.34 kwa nchi ya Kenya. Kitita hicho kilitolewa kwa minjili ya kuwezesha Nairobi kupambana dhidi ya janga la Covid-19 na kuepusha hatari ya kuwa na deni kubwa. Lakini, tangu tangazo la Aprili 2, ukosoaji umekuwa ukiongezeka kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mitandao ya kijamii, wengi wamelitaka shirika la Fedha la Kimataifa , IMF, kuacha kukopesha Kenya, hali ambayo imefanya gumzo katika siku za hivi karibuni. Wakosoaji wanatoa wito moja kwa moja kwa IMF. Pia wameiomba IMF kusimamishaufadhili wake mpya ambao unaendana na msaada wa dola milioni 739 ambazo zilitolewa mnamo mwezi Mei 2020. Ombi hili la mkondoni pia limetiwa saini na zaidi ya watu 220,000.

Ukosefu wa uwazi na ubadhirifu

Nakala hiyo inalaani ukosefu wa uwazi wa mamlaka ya Kenya katika matumizi ya mikopo ya kimataifa. Kashfa kadhaa za ufisadi zimeibuka katika miezi ya hivi karibuni. Kesi ya utapeli ya dola milioni 70 hasa inalenga shirika la ununuzi wa vifaa vya matibabu, KEMSA, ambalo linalaumiwa kwa gharama zinazohusiana na vita dhidi ya Covid-19.