TANZANIA

Tanzania na Burundi zashtumiwa mauaji na mateso kwa wakimbizi wa Burundi

Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania Juni 11, 2015.
Wakimbizi wa Burundi wakisubiri kuingia katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu kaskazini mwa Tanzania Juni 11, 2015. AFP PHOTO/STEPHANIE AGLIETTI

Umoja wa mataifa umezitaka nchi ya Burundi na Tanzania, kuheshimu haki za wakimbizi wanaokimbia mauaji na mateso nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Takwimu za Umoja wa Mataifa, zinaonesha kuwa raia wa Burundi zaidi ya laki tatu walikimbia  nchi yao kufuatia machafuko ya kisiasa mwaka 2015 yaliyozuka baada ya aliyekuwa rais Hayati  Pierre Nkuzunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Aidha, ripoti hiyo inaeleza  polisi nchini Tanzania na maafisa wa idara wa ujasusi wameendelea kuwakamata na kuwapoteza wakimbizi hao wakishirikiana na wenzao kutoka Burundi.

Wakimbizi warudishwa nyumbani kwa nguvu

Baadhi ya wakimbizi wamedai kukamatwa usiku wa manane kwenye kambi na maofisa wa polisi, waliojifanya wakimbizi na kuingia ndani ya kambi za wakimbizi, wengine wakilazimishwa kurudi nyumbani.

Kumekuwa na mchakato wa kuwarudisha nyumbani wakimbizi hao wa Burundi, baada ya serikali yao kusemla amanina utulivu zimerejea lakini wakimbizi waliowengi wanaonekana kutokuwa tayari kurejea nyumbani kwa kile wanachosema wanahofia usalama wao.