SUDANI KUSINI

Ripoti : Kuna hatari Sudan kutumbukiwa tena katika vita vya webyewe kwa wenyewe

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake Riek Machar katika Ikulu ya rais huko Juba Aprili 26, 2016.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Makamu wake Riek Machar katika Ikulu ya rais huko Juba Aprili 26, 2016. REUTERS/Stringer

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini, inaonya kuwa kutokutekeleza kikamilifu mkataba wa amani wa mwaka 2018 unaweka nchi hiyo kwenye hatari ya kurejea kwenye mzozo mkubwa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo ambayo imekabidhiwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, imesisitiza haja ya mashauriano ya dharura ili kuzuia uwezekano mkubwa wa nchi hiyo kutumbukia kwa mara nyingine kwenye mzozo.

Watalaam wamependekeza kuendeleza marufuku ya silaha iliyowekewa nchi hiyo na Umoja wa Mataifa, ambayo muda wake unatazamiwa kumalizika mwezi Mei  na kuwekewa vikwazo wote wanaozuia msaada kuwafikia walengwa nchini humo.

Tangu mwezi Februari, utekelezwaji mkataba wa amani, umeendelea kukwama, huku tofauti zikishuhudiwa katika chama cha SPLM kwa tawi linaloongozwa na rais Salva Kiir na upande unaongozwa na makamu wa kwanza wa rais Riek Machar.

Umoja huo pia umesema watu zaidi ya Milioni 8 wanakabiliwa na baa la njaa, na wanahitaji msaada wa haraka.