BURUNDI

Wafungwa zaidi ya 3,000waachiliwa huru kwa msamaha wa rais Burundi

Baadhi ya wafungwa katika jela kuu la Mpimba wakifuata kwa makini hotuba ya rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Aprili 26, 2021.
Baadhi ya wafungwa katika jela kuu la Mpimba wakifuata kwa makini hotuba ya rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, Aprili 26, 2021. REUTERS - EVRARD NGENDAKUMANA

Nchini Burundi, wafungwa zaidi ya Elfu Tatu kati ya 5,255 waliopewa msamaha wa rais mwezi Machi wameachiliwa huru, huku rais Evariste Ndayishimiye akikanusha kuwepo kwa wafungwa kisiasa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Katika jela kuu ya Mpimba inayopatikana kusini mwa mji wa Bujumbura wameachiliwa huru wafungwa 944 wakiwemo wanawake 23. Rais wa Burundi, Evariste Ndaishimiye ameongoza sherehe za kuwaachilia huru wafungwa hao waliopewa msamaha. Na katika hutuba yake ametupilia mbali madai ya kuwa kuna wafungwa wa siasa.  

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye awasili kwa ajili ya uzinduzi wa kutoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3,000 katika jela kuu la Mpimba, kama sehemu ya juhudi za kupunguza msongamano katika magereza, Bujumbura, Burundi Aprili 26, 2021.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye awasili kwa ajili ya uzinduzi wa kutoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 3,000 katika jela kuu la Mpimba, kama sehemu ya juhudi za kupunguza msongamano katika magereza, Bujumbura, Burundi Aprili 26, 2021. REUTERS - EVRARD NGENDAKUMANA
Anaedai kuwa ni mfungwa wa kisiasa, anitumie barua, na anipe ufafanuzi wa madai yake ili nichunguze sheria inasemaje, iwapo ni siasa au makosa aliyoyafanya. Watu wanaambatanisha mambo. Mwanachama akimjeruhi mtu, kwa sababu ni mkereketwa wa chama fulani, utamsikia mku wa chama hicho akibaini kuwa mufuasi wake ametiwa ndani kutokana na sababu za kisiasa. Siasa gani? Alitiwa jela kwa tuhuma ya kumjeruhi mtu

Licha ya hayo wawakilishi wa mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini Burundi waishio uhamishoni kufuatia mzozo wa mwaka 2015, wanazidi kuomba wafungwa wa kisiasa wasamehewe. Baadhi ya wafungwa hao unakutana wanakabiliwa na tuhuma ya kuyumbisha usalama wa nchi, na msamaha huo wa Rais wa Jamhuri ya Burundi hauwahusu wafungwa hao.