UGANDA-ICC

Uganda: Hatma ya kiongozi wa waasi Ongwen kujulikana Alhamisi hii

Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016
Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016 ICC media outlet

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatarajia leo Alhamisi kutangaza hukumu iliyotolewa kwa Dominic Ongwen, mwanajeshi mtoto wa zamani wa Uganda ambaye alikua kamanda wa kundi la waasi wa Lord Resistance Army (LRA), aliyepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Dominic Ongwen, 45, anakabiliwa na kifungo cha maisha baada ya kupatikana hatiani mwezi Februari kwa mashtaka 61, ikiwa ni pamoja na ubakaji uliokithiri dhidi ya wanawake na wasichana, kosa ambalo hadi sasa halijatangazwa na ICC yenye makao yake Hague.

Alipatikana pia na hatia ya mauaji, ubakaji, utumwa wa kijinsia na kuwasajiliwa kwa nguvu watoto kujiunga na kundi hilola waasi.

Kulingana na mahakama, Bwana Ongwen aliamuru kushambuliwa kwa kambi za wakimbizi mwanzoni mwa miaka ya 2000, wakati alikuwa mmoja wa makamanda wa LRA, kundi lenye silaha linaloongozwa na mbabe wa kivita Joseph Kony, ambaye aliongoza vita vya kinyama nchini Uganda na katika nchi tatu jirani ili kuunda taifa litakalofuata misingi na amri kumi za Biblia.