TANZANIA-AFYA

Tanzania: Rais Samia Suluhu Hassan achukua hatua za kudhibiti Covid-19

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Machi 16, 2021.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Machi 16, 2021. AP

Kutokana na kuwasili kwa aina mpya ya kirusi cha Corona katika bara la Afrika, Tanzania imetangaza hatua za kukabiliana na janga hilo hatari ambalo limesababisha maafa makubwa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hii, ambapo neno "coronavirus" lilikuwa mwiko katika miezi iliyopita, wiki hii ilitangaza masharti mapya ya kusafiri katika mlrngo la kuzuia kuenea kwa janga hilo.

Aina hii mpya ya kirusi cha Corona kutoka India ni moja ya sababu kuu kwa uamuzi huu, lakini pia inaonyesha nia ya rais mpya, Samia Suluhu Hassan, kukabiliana na janga hili tofauti na mtangulizi wake Hayati John Pombe Joseph Magufuli.

Rais mpya wa Tanzania wiki hii alipiga marufuku safari zote za ndege kwenda na kutoka India ambapo aina mpya ya kirusi cha Corona imeitumbukiza nchi hiyo katika mgogoro mkubwa wa kiafya. Aina hii mpya ya kirusi cha Corona inazunguka katika nchi tatu za Kiafrika zikiwemo nchi jirani za Uganda na Kenya.

Ili kuepusha kirusi hiki kuingia nchini Tanzania, Wizara ya Afya ya ncini humo imetangaza udhibiti mkali kwa wasafiri kutoka nchi zilizo hatarini, na wasafiri kulazimishwa kuingia karantini ya lazima wanapowasili kwa siku 14, kwa gharama zao.