TANZANIA

Lissu asema serikali mpya nchini Tanzania haijaleta mabadiliko

Mwanasiasa wa upinzani  nchini Tanzania Tundu Lissu.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu. AFP

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu anayeishi uhamishoni nchini Ubelgiji, katika mazungumzo maalum na RFI amesema serikali mpya ya rais Samia Suluhu Hassan, haifanyi vya kutosha kujitofautisha na ile ya mtangulizi wake Marehemu John Magufuli kuhusu masuala mbalimbali hasa uhuru wa kidemokrasia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Je, atarudi Tanzania hivi karibuni na nini maoni yake kuhusu mbinu za rais Samia kupambana na janga la Covid 19.

Sikiliza mahojiano haya yaliyowezeshwa na mwandishi wa RFI Kifaransa Christina Okello.  Maswali yameulizwa na Ruben Lukumbuka.