KENYA-SIASA

Mageuzi ya katiba Kenya: Serikali yakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu

Jaji Martha Koomekatika mahojiano kuhusu uteuzi wake kwenye nafasi ya jaji mkuu wa Mahakama Kuu Nairobi, Kenya, Aprili 14, 2021.
Jaji Martha Koomekatika mahojiano kuhusu uteuzi wake kwenye nafasi ya jaji mkuu wa Mahakama Kuu Nairobi, Kenya, Aprili 14, 2021. via REUTERS - JUDICIAL SERVICE COMMISSION

Nchini Kenya, baada ya Mahakama Kuu kuamua wiki iliyopita kuwa mchakato wa mageuzi ya Katiba, BBI, haukuwa halali kisheria, mwanasheria mkuu wa serikali amekataa rufaa, kutaka uamuzi huo kubadilishwa.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Mahakama wiki iliyopita na uamuzi wa serikali kukataa rufaa, umezua mitazamo mbalilbali miongoni mwa wakazi wa jiji la Nairobi.  

Hilo jambo sijalipokea kwa uzuri kwa maana tunataka katiba iweze kufanyiwa marekebisho ili tuweze kupata nafasi nyingi hasa kuhusu swala hili la uchaguzi limekuwa ni kizungumkuti sana.

BBI yenyewe hata hatukupewa nakala tusome, ni hawa hawa wanasiasa ambao wanshiriki katika mikutano yao wakiambia watu kwamba BBI ni zuri.

Joseph Simekha, Mtaalamu wa masuala ya haki na uongozi nchini Kenya, anasema uamuzi wa Mahakama Kuu ni kukosa heshima kwa ofisi ya rais.

Sidhani kama uamuzi huo unaweza kuzua mzozo kwa sababu hiyo ni kazi ya Mahakama na Mahakama inafanya kazi yake na sio kila wakati mahakama ikichukuwa uamuzi unaofurahisha kila mtu na wale ambao hawakufurahishwa na uamuzi wa mahakama wanatakiwa kukata rufaa au wakubali matokeo.

Hata hivyo, Gad Gathu wakili wa Mahakama kuu, kwa upande wake, anaona Majaji walitoa maamuzi sahihi.

Mahakama kwa upande mkubwa waliweza kufanya ipasavyo kuzuia ule mchakato wa BBI kuendela na waliweza kupeana sababu muhimu sana, kwa hiyo hukumu ambayo walitoa kwa hivyo, sidhani kwamba walifanya vabaya.

Kinachosalia sasa ni kuona kama Mahakama ya rufaa, itabadilisha uamuzi wa Mahakama Kuu ili kuokoa mchakato wa mageuzi ya Katiba nchini Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.